Ukraine wathibitisha wanajeshi wake kuuawa

0
Rais Volodymyr Zelensky .

UKRAINE imethibitisha kwamba wanajeshi wake 19 wameuwawa katika shambulio la makombora la Urusi lililofanywa katika mji wa Zaporizhizhia wakati wa sherehe ya kuwatunukia tuzo wanajeshi.

Rais Volodymyr Zelensky amesisitiza kwamba tukio hilo la mauaji lingeweza kuepukika.

Waziri wa ulinzi Rustem Umerov ametoa maagizo ya kufanyika uchunguzi kuhusu tukio hilo kubaini kwanini brigadia maalum ya jeshi la operesheni za milimani ilishiriki katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na watu wengi Ijumaa iliyopita.

Tangazo hilo limekuja wakati maafisa wakiripoti kutokea mashambulizi yaliyofanywa na ndege isiyokuwa na rubani ya Urusi pamoja na makombora na kujeruhi watu wanane na kuharibu jengo la makumbusho ya sanaa ambayo ni sehemu ya turathi za dunia zilizoorodheshwa na shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here