JOHANESBURG, Afrika Kusini
SERIKALI ya Afrika Kusini imewaita nyumbani balozi wake na ujumbe wake wa Kidiplomasia kutoka Israel, katika hatua ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na nchi hiyo dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuyaita ni mauaji ya halaiki.
Mbali na hatua hiyo, Serikali ya Afrika Kusini pia imetishia kuchukua hatua dhidi ya balozi wa Israel nchini mwake kufuatia matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kuhusu msimamo wa nchi hiyo ya Afrika katika vita kati ya Israel na Hamas.
Waziri wa Afrika Kusini katika ofisi ya rais Khumbudzo Ntshavheni Afrika Kusini imeamuwa kuwaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Tel Aviv kwaajili ya mashauriano.
Waziri wa Mambo ya nje Naledi Pandor ambaye hivi karibuni amemkaribisha mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba, alisema wanahitaji kushauriana na wanadiplomasia hao waliokuwa Tel Aviv kutokana na hali ya mauaji ya watoto inayowatia wasiwasi katika Ukanda wa Gaza.