UN walilaani kundi la Hamas

0
Antonio Guterres, United Nations High Commissioner for Refugees speaks during a press conference at the Launch of the Regional Flash Appeal Following recent events in Libyan Arab Jamahiri

NEW YORK, Marekani

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameieleza hali katika Ukanda wa Gaza kuwa janga la kibinadamu ambapo hali ni ya wasiwasi mjini Jerusalem, Ukingo wa Magharibi na kwenye mpaka baina ya Israel na Lebanon.

Akizungumza na waandishi habari mjini New York, Guterres alisema operesheni ya ardhini ya jeshi la Israel na mashambulizi ya mabomu yanayoendelea yanawaathiri raia, hospitali, kambi za wakimbizi, misikiti, makanisa na vifaa vya umoja wa Mataifa yakiwemo makazi.

Alisema, wakati huo huo Hamas na wanamgambo wengine wanawatumia raia kama ngao ya binadamu kujilinda na wanaendelea kuvurumisha maroketi kiholela kuelekea Israel.

Aidha, alisema malori takribani 400 ya mahitaji ya misaada yamefanikiwa kuingia Ukanda wa Gaza katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Kabla vita kuanza malori kiasi 500 yalikuwa yakiingia Gaza kila siku.

Guterres aliongeza kuwa, mafuta yanayohitajika kwa dharura na ambayo ni muhimu kuendeshea shughuli katika hospitali, hayakuweza kusafirishwa kufika Gaza, akiitaja Gaza kama kaburi kwa watoto.

Hadi sasa, taarifa zinaonyesha kuwa, idadi ya Wapalestina waliouliwa Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7 kati ya Israel na kundi la Hamas, linalotambuliwa kama la kigaidi nchini Ujerumani, Marekani na Umoja wa Ulaya, imepanda hadi kufikia 10,022.

Kwa mujibu wa wizara ya afya inayodhibitiwa na kundi hilo inasema, maelfu ya wanawake na vijana ni miongoni mwa wale waliuouliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya kutokea angani na ya ardhini ya Israel.

Guterres amelilaani kundi la Hamas kwa vitendo vyake vya kigaidi na kurudia wito wake kutaka zaidi ya mateka 200 ambao wamekuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza kwa mwezi mmoja sasa, waachiwe huru mara moja.

Pia, alisema usitishwaji mapigano kuruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu sharti utekelezwe na Israel na watawala wa Hamas huko Gaza ili kufikisha mwisho jinamizi la vita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here