Wasomi ambao hawakuandaliwa, ni hasara kwa Mataifa yao

0

Na Prof. Dkt. Kudret BÜLBÜL 

MIAKA ya nyuma, watafiti wa Kimagharibi walikuwa wakifunga safari na kwenda kufanya tafiti kiuhalisia wao wenyewe katika jamii za Mashariki.

Hivi sasa ni kwamba, Mataifa hayo yanawatumia wasomi kutoka nje ya Magharibi wanaokwenda kwa ajili ya masomo katika Mataifa yao.

Tuliona jinsi Mataifa yanavyotumia mali zao kusomesha wasomi wao nje ya nchi na jinsi wasomi hawa wanavyobadilika na kuwa wasomi kwa manufaa ya Mataifa ya Kimagharibi waliosemeshwa kwa kugharamiwa na Mataifa yao. Hii ni hasara kwa Mataifa wanayotoka.

Wasomi ambao hawakuandaliwa kwa ajili ya nchi zao wanazotoka, ni vigumu kutoa mchango wowote katika maendeleo ya Mataifa yao husika pindi wanaporudi, hilo limekuwa tatizo kwa zaidi ya miaka 200.

Katika hali kama hii, gharama zilizotumiwa na Mataifa husika kuwasomesha wasomi hawa nje ya nchi zao inakuwa zimetumika bure bila kuwa na faida yoyote.

Wasomi ambao wamesomeshwa nje ya nchi zao kwa madhumuni kwamba wakirudi wazisaidie nchi zao katika kuleta maendeleo, hawakidhi dhumuni hilo kwa kuwa wakirudi katika nchi zao wanakuwa wakihudumia Mataifa ya Magharibi.

Wasomi hawa waliofuzu ambao wameandaliwa kwa ajili ya kuyahudumia Mataifa ya Magharibi, ingawa inakuwa ni nguvu kazi iliyofuzu kielimu katika nchi wanayotoka, ila wanakuwa wamefuzu kimitazamo ya Kimagharibi.

Tukilitazama hili kwa kuiangalia Uturuki. Je, tunaweza kusema kwamba hii si mojawapo ya sababu za msingi za kuwako kwa fikra za Kimagharibi miongoni mwa wasomi wetu kwa miaka 200?.

Kupata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi haswa unapokuwa umetoka katika nchi za dunia ya tatu ni faida kubwa. Faida hii kwa wanaoipata hujionyesha pale wanaporejea katika nchi zao, watu hawa huchukuliwa kwa uzito wa aina yake.

Ndio maana, pale watu hao walioelimishwa kwa faida ya nchi walizoelimishwa na sio nchi wanazotoka wanaporudi makwao, athari zinazoweza kusababishwa na watu hawa zinakuwa kubwa sana.

Ni karibu miaka 100 sasa tangu Waziri mkuu wa dola ya Othoman, Said Halim Paşa, alipozungumzia kadhia hii, na hii inaonyesha kwamba, tatizo hili sio jipya.

Katika kipindi alichoishi Paşa, alizungumzia kwa kuwalinganisha ni wapi wana madhara zaidi kati ya wasomi ambao hawana maarifa juu ya nchi zao na wale ambao hawana maarifa juu ya Mataifa ya Magharibi.

Alisema, wote wana madhara, lakini wale ambao wana maarifa juu ya masuala ya Magharibi, hawana maarifa juu ya nchi zao; hao ndio wana madhara zaidi.

Watu ambao wameishi nje ya nchi zao kwa muda mrefu, wanageuka na kuwa wanazitazama nchi zao wanazotoka kama nchi za kigeni. Kitu kinachowafanya watu hawa wakae mbali na masuala yanayozihusu nchi zao.

Kwa wale wanaorejea katika nchi zao kutoka Mataifa ya nje, kinachohitajika kutoka kwao sio kuanza kuorodhesha matatizo ya nchi zao ambazo kwa mara nyingi yanakuwa yanafahamika na kila mtu, bali kinachohitajika ni kutoa suluhisho la matatizo hayo kwa ustadi.

Theoria za elimu ya nchi walizoenda kupata elimu inabidi wazifanyie upembuzi yakinifu kuona ni jinsi gani zinakidhi kutatua matatizo ya nchi wanazotoka.

WASOMI WADUMISHE UZAWA WAO

Watu ambao wametumwa na Mashirika ya umma wakafanye utafiti kwa ajili ya Mashirika yao wanapofanya utafiti kwa ajili ya taasisi za elimu za nje wanazokwenda,  watu hawa matokeo yao huziona jamii zao wanazotoka kama za ajabu.

Kutokana na hilo, hawa huwa ni hasara kubwa kwa wanataaluma wa kizazi kijacho, kwa kuwa watu hawa hurithisha mtizamo huo kwa kizazi hicho.

Elimu inayotolewa katika Mataifa ya Magharibi hasa katika upande wa sayansi ya jamii bila shaka ina maana kubwa kwa nchi hizo. Kwa kiasi fulani elimu hii pia inaweza kuwa na manufaa kwa nchi nyingine.

Lakini, pale inapotokea wanataaluma hasa katika kada za siasa, uchumi, Sosiolojia na aina nyingine ya elimu ya kijamii wanapotoa elimu vilevile kama nchi za Magharibi wanakuwa wanaharibu historia na mizizi ya nchi zao husika.

Hii ni kwa sababu, maandiko ya vitabu vya Magharibi mara nyingi huwa hayatoi nafasi kwa maarifa au elimu ya nje ya Magharibi.

Kinachotegemewa ni kwamba, wasomi kutoka nje ya Magharibi wachukue elimu ya Magharibi waipembue kulingana na historia na hali katika nchi zao ndipo waitumie katika nchi zao.

Wasomi hao wanaposhindwa kufanya hayo, hatuwezi kuzilaumu nchi za Magharibi kwamba ndio zimehusika kuharibu historia na elimu za nchi husika, bali ni hao wasomi wa nchi husika kwa uvivu wa kifikra wameshindwa kuchukua elimu ya Magharibi na kuifanyia upembuzi yakinifu ifae katika mazingira ya nchi zao bila kuharibu historia, tamaduni na elimu za nchi zao.

VYANZO VYA TATIZO

Bila shaka katika wasomi wanaounda nchi za ng’ambo wapo ambao hufanya tafiti za thamani kwa ajili ya Mataifa yao. Tukiwaondoa hao tunaweza kusema chanzo cha tatizo ni kama ifuatavyo:-Kutokuwepo kwa mipaka katika aina ya elimu na nchi wanazoenda kusoma watu wetu.

Iwe ni kwa wanataaluma wanaotumwa na vyuo vikuu au wale wanaotumwa na taasisi za umma kwa ajili ya elimu nje ya nchi, hakuna mipaka inayowekwa. Mara nyingi uamuzi wa fani na hata nchi huachwa mikononi mwa msomi husika.

Kutafuta urahisi kwa upande wa wanaoenda kusoma ng’ambo, mara nyingi kwa wasomi wanaenda kusoma nje ya nchi zao inabidi wafanye tafiti kuhusiana na nchi hizo wanazokwenda, hivyo inawapasa watu hao waifahamu vizuri lugha za nchi hizo wanazokwenda sambamba na hilo inawabidi kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Hii ni kwa sababu wapo wanafanya utafiti katika mazingira ya wanataaluma ambao wana elimu zaidi katika mada husika na ni wazawa wa nchi hizo. Lakini, sio lazima watu hawa wachague mada zinazohusiana na nchi wanazoenda kutafuta elimu.

Kwa ajili ya kutafuta wepesi au labda kufuata maelekezo mabaya nimeshuhudia kazi nyingi za watahiniwa wa shahada ya uzamivu (PHD) ambazo hazina manufaa yeyote kwa nchi zao.

Nchini Australia mwanafunzi mmoja alifanya tasnifu inayohusu siasa za Uturuki juu ya Umoja wa Ulaya. Mwingine nchini Ujerumani alifanya tasnifu inayohusu chama cha siasa cha AK parti, wote hawa walisema lengo leo ni kurudi Uturuki.  

Niliwaambia, Uturuki inahitaji wahitimu wa shahada za uzamivu kutoka nje ya nchi, lakini tasnifu walizofanya hata watu wa mtaani nchini Uturuki ni wabobezi katika mada hizo.

Nikawauliza tasnifu zenu zitaisaidia vipi Uturuki, zitatoa mchango gani katika maendeleo ya Uturuki. Kufanya tasnifu inayohusu masuala ya Ulaya, ina maana sana kwa watu wa Ulaya; ni kwa sababu hiyo nikawaambia kazi zao zitakuwa na faida zaidi kwa Ulaya.

Mwaka 2017 nchini Marekani, nilikutana na mada mbili za tasnifu za shahada ya uzamivu ambazo zimeandaliwa kimtindo huu tunaouzungumzia. Ingawa sikuweza kuwashawishi, lakini niliwaambia yafuatayo, “Mnatagemea mtakaporudi Uturuki kazi zenu hizo za kitaaluma zitaisaidiaje nchi yenu?.

Kama mngefanya utafiti juu ya uhusiano uliopo baina ya serikali ya Marekani na dini, au juu ya elimu ya kueneza Injili (Evanjelism) tasnifu zenu zingekuwa na faida na uhitajika mkubwa zaidi.”

Kupatiwa ushauri na wanataaluma wenye mitazamo ya kibeberu katika nchi wanazoenda, mara nyingine aina hii ya ushauri pia huwa na madhara, lakini si kwa yule ambaye anajua kilichompeleka katika nchi hizo, aina hii ya ushauri kwake si kikwazo kisicho weza kuvukika.

Wakati natafuta shahada ya uzamivu nilifanya usahili katika chuo kimoja nchini Uingereza. Katika usahili huo niliwaambia nataka kufanya utafiti katika masuala yanayohusu Uingereza.

Walisema ni kama bahati kwa mara ya kwanza wamepata pendekezo kutoka kwa mwanafunzi anayetokea Mashariki na kulikubali pendekezo langu. Bila shaka katika baadhi ya mada zinahitajika tafiti za waturuki hata tunaweza kusema zinaweza kuzaminiwa.

Historia ya Uturuki kwa kiasi kikubwa inahusiana na dola la Othman. Bila shaka urithi huu inabidi uelezewe dunia nzima kwa tafiti zilizofanywa na Waturuki wenyewe katika hali ambayo sio ya kupotosha.

Watafiti wanaotaka kufanya tafiti kuhusu Uturuki tofauti na eneo kama hilo inabidi wapate ruhusa kutoka kwa taasisi zinazowatuma nje. Tukifanya hivyo tutakuwa tumetatua tatizo lililotukabili kwa miaka 200.

Uanzishwe utaratibu maalum kwa taasisi zinazopeleka wataalamu kusoma nje ya nchi zitakazowataka wataalamu hao wafanye tafiti zitazoisaidia Uturuki na hata nchi nyingine. Hii itaweka kinga dhidi ya tatizo lililopo.

Kinyume na hivyo, tutaendelea kupotea kwa watafiti wetu kufanya tafiti kwa niaba ya nchi za Magharibi kama vile isemavyo simulizi kwa mtindo wa shairi ya Sezai Karakoç.

*Mwandishi wa Makala hii ni Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa wa Chuo Kikuu cha Ankara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here