Mwanazuoni aliyepigania dunia kuwa sehemu inayomfaa binadamu kuishi kwa amani

0

Na Habib Miradji

MWANAZUONI na mhubiri wa dini ya Kiislamu Mohamedi Fethulaah Gulen (83) amefariki dunia akiwa anapata matibabu kwenye hospitali moja akiwa uhamishoni nchini Marekani.

Fethullah Gulen mwanatheolojia wa dini ya kiislam alikuwa miongoni mwa watu 100 mwa wenye uweledi na jarida la FOREIGN POLICY and Prospect mchango mkubwa duniani kuwaunganisha watu wa Mataifa mbalimbali kwa kuhubiri amani, vita dhidi ya umaskini, ujinga maradhi na utengamano.

Gulein Raia wa Uturuki anatajwa kuwa Mahubiri yake na vitabu vya dini kiislam, na ujenzi wa familia, Elimu, demokrasi na mambo ya kijamii vimempatia wafuasi wengi duniani kote wanaojulikana kwa jina la Hizmet au Gulen Movement. Mtandao ulioenea nchi mbali mbali ncni barani Marekani, America ya kusini, Ulaya, Asia na Afrika.

Hizmet kwa Kiswahili Huduma ni Mtandao uliweza kujenga shule na vyuo nchini Uturuki na msisitizo katika masomo ya sayansi na hesabu Mtandao wake wa Hizet ukasambaa barani Ulaya bara la Amerika Afrika na Asia huku na vijana wengi dini tofauti kuhamashiwa masomo ya sayansi na hisabati.

Nchini Uturuki mtandao huu mbali na kujenga mashule ya kisasa vyuo vikuu vya tiba, na kujenga mahositali, vyuo ya ujenzi na teknolojia. Wafuasi wa Guleni walifungua makampuni na vyombo vya Habari vikiwemo redio na Televisheni na viwanda vya uchapishaji kwa ajili ya kuhamasisha mtandoni duniani na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Marehemu Ali Hassani Mwinyi Alipokwenda kwenye mkutano wa HABITAT mwaka 1996 alitembelea moja ya shule hizo za kisasa alipokutana viongozi wa Hizmet aliwomba kuja kuwekeza hapa nchini na kuja hapa mwaka 1997.

Toka mwaka huo chini ya Hizmet Tanzania imefanikiwa kuwa na Shule za Feza Boys High School, Feza Girls Feza internation na Shamsye za jijini Dar es salaam Feza Zanzibar na Feza Dodoma shule hizi ni jukwaa la kuwalea Watoto wa dini mbalimbali na tamaduni mbalimbali.

Nchini mbalimbali za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya Uganda Rwanda Zambia na Afrika za Kusini Somalia Sudani Msumbiji na DR Congo, mitandao wa Hizmet umejenga shule zinazotoa huduma kwa wananchi wa nchi hizo.

Hadi anafariki Gulen aliwahimiza wafuasi kukaa mbali na mambo ya siasa. Kutokana na kuwa na wafuasi wengi mno ndani na nje ya Uturuki wanasiasa nchini humo walijenga urafiki na Gulen watumie mtandao wake kupata kura.

Rais Recep Tayyip Erdoğan na chama chake cha siasa AKP kinachotawala sasa nchini Uturuki walikuwa na urafiki mkuu wa Gulen nia yake kuwatumia mtandao wa Gulen kupata kura na hatimaye kushinda uchaguzi uliomweka Erdogan madarakani.

Erdogan na hatimaye kuwa Rais wa nchi hiyo, nguvu kubwa ya hizmet iliyowekezwa kwenye elimu ilitoa wanafunzi bora walioajiriwa kwenye nyaja zote polisi wanajeshi, wanasheria majaji waalimu madaktari na watalamu IT Haya yalimtisha Erdogan kuhakikisha anasambaratisha mtandao wa Gulen.

Uhasama kati ya Gulen na Erdogan ulifikia kilele wakati serikali ya Uturuki ulipomshtumu Gulen kupanga jaribio la kupindua serikali ya nchi hiyo la July 15, 2016 Hizment litangazwa ni kundi la kigaidi na kutangaza kupambana nalo ndani na nje.

Shule zote vyuo vikuu, NGOs, benki magazeti makampuni ya wafuasi wa Gulen, televisheni radio na vyama vya kitaaluma vilichukuliwa na serikali ya vingine kufungwa kabisa Wafuasi wa Hizment wengi wapo magerezani wakihushwa na ugaidi

Kuna msemo maarufu hapa duniani usemao hivi Ukitaka kumuua mbwa kwanza umpatie jina baya, Gulen na mtandao wake wamepewa jina la ugaidi ili kuwafitinisha na dunia, lakini hakuna gaidi duniani anayeweza kujenga shule, kuhamisha maskini na matajiri kusoma bila ubaguzi wa dini rangi au utaifa.

Majaji Maprofesa, wanajeshi polisi waliondolewa kwenye kazi zao na kupelekwa magerezani na wengine wamekimbia nchi ya na kwenda uhamishoni. Walimu zaidi ya 20,000 waliipitia kwenye shule za Hizmet wamefutiwa leseni za kufundishia.

Gulen mwenyewe amekuwa akiishi uhamishoni Marekani toka 1999, alikanusha yeye na mtando wake hawakuhusisha na jaribio la kufanya mapinduzi na wao si magaidi na kusisitiza hizmet inaendelea kujenga maelewano miongoni mwa wafuasi wa dini zote kwa misingi ya kuvumilina na kustamiliana.

Moja ya nukuu za falsa za marehemu Fethullah Gulen ni kudai kuwa “Uvumilivu hufanya moyo wa mtu kuwa mpana kama bahari na huvutia imani na upendo kwa watu wengine, kuwasaidia wenye shida na kuwajali kwa mali na mali.”

Tunaendelea kumkumbuka Gulen licha ya kuwa mhubiri kwa Kiislam mwenye falsafa pana kuijenga dunia kwa uwiano na dini zote na kumfaa mwanaadamu kuuishi kwa amani.

Dunia nzima tayari imeonja falsafa za Gulen moto aliouanzisha na mtandao wake wa Hizmet hauwezi kuzimwa na wapinzani kwani ni sawa ana kutwanga pilipili kwenye kinu ambapo mshahara ni kukohoa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here