Idadi ya wanaohitaji chakula kuongezeka zaidi Kenya

0

NAIROBI, Kenya

KENYA imesema idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula nchini humo huenda ikaongezeka kutoka Milioni 4.3 wa sasa kutokana na ukame unaoendelea.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Ukame ya Kenya (NDMA) Hared Adan, alisema mjini Nairobi kuwa mvua zinazoripotiwa zinatarajiwa tu kuongeza vyanzo vya maji na kuotesha malisho katika maeneo yenye ukame na ardhi nusu kame (ASAL).

“Majira ya kiangazi ya Januari hadi Machi 2023 huenda yakabadilisha ahueni yoyote inayoshuhudiwa sasa,”

Adan pia alisema, matatizo ya ukame huenda yakaongezeka tena mwakani, kwa hiyo mwitikio wa dharura kwa ajili ya ukame unahitajika, kwenye kaunti 13 ambazo ziko katika hatua ya tahadhari huku nyingine saba zikiwa katika kipindi cha hatari ya ukame.

Pia, alisema moja ya athari kuu za ukame ni vifo vya mifugo inayokadiriwa kufikia Milioni 2.5 katika kaunti zenye ukame.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here