Na OR-TAMISEMI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema Halmashauri ya Mwanga imeandaa andiko lenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.2 na kuliwasilisha Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa wilayani humo.
Dkt. Dugange ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha sita mkutano wa 13 unaoendelea jijini Dodoma.
“Mhe Spika Serikali inatambua ufinyu wa stendi ya magari katika Halmashauri ya Mwanga lakini tayari Ofisi ya Rais-TAMISEMI tumepokea andiko lenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.2 tokea Agosti mwaka huu na hatua iliyopo hivi sasa ni ya watalaamu wetu wizarani kuendelea na mapitio ya andiko hilo kulingana na vigezo,” alisema Dkt. Dugange.