MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umefafanua utaratibu wa utekelezaji wa mradi wa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa walimu wa shule za sekondari za umma, unaolenga kuwawezesha walimu kutumia, kusimamia na kutunza vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Serikali kupitia UCSAF kwa ajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa UCSAF ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatekelezwa kwa ushirikiano na vyuo vikuu, ambapo walimu wanapatiwa mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya TEHAMA pamoja na namna ya kuvitunza ili viendelee kutoa huduma iliyokusudiwa kwa muda mrefu.
#UCSAF #MawasilianoKwaWote #MafunzoYaTEHAMAKwaWalimu