SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) limeamua kurejesha mfumo wa kuandaa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kila baada ya miaka miwili.
Uamuzi huo umefikiwa kwa kauli moja na kamati ya utendaji ya CAF (EXCO), na kurejesha utaratibu uliokuwa ukitumika kabla ya pendekezo la kubadilisha michuano hiyo na kuifanya ifanyike kila baada ya miaka minne.
Rais wa CAF, Patrice Motsepe, alikuwa ametangaza katika mkutano wa mkakati wa shirikisho hilo uliofanyika Cabo Verde kuanzia Oktoba 7 hadi 9 mwaka 2026, kwamba kamati ya utendaji ingepitia upya uamuzi wa awali wa kuandaa AFCON kila baada ya miaka minne.
CAF imesema miongoni mwa sababu za kubadili msimamo huo ni kwamba mashindano mapya ya Afrika, yaliyopendekezwa kwa jina la Africa Nations League, yatahitaji miaka kadhaa kabla ya kuanza kuzalisha mapato makubwa yanayoweza kugharamia mashindano ya CAF na kusaidia kukuza ushindani wa soka la Afrika kimataifa.