MCHEZAJI nyota wa zamani wa mpira wa miguu aliyeichezea Chelsea FC na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba anatarajiwa kuwasili Tanzania.
Drogba anawasili nchini Tanzania, kuangalia maandalizi ya nchi hiyo, inapojiandaa kuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON 2027.
Mwezi Mei mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, alikutana na Drogba na kumwomba kuwa Balozi Maalum wa Tanzania kuelekea fainali hizo, mwakani.
Michuano ya AFCON 2027, inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.