Rais Mwinyi: Tusimamie malezi na maadili ya vijana na watoto

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezitaka familia kuweka dhamira ya Kusimamia Malezi ya Vijana na Watoto ili kuwa na Taifa lenye Heshima na Maadili.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Masjid Al Sahar Kwarara, Njia nne, Mkoa wa Mjini Magharibi Mei 2, 2025.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alisema mambo mengi yanayojiri hivi sasa ndani ya Jamii yakiwemo ya Wizi na Uharibifu wa Miundonbinu ya Serikali yanafanywa na Vijana waliokosa Malezi Bora na Maadili ya Dini.

Amefahamisha kuwa Mustakabali wa Nchi yoyote Unahitaji Malezi ya Vijana na Watoto waliolelewa kwa Maadili Ili kuwa Watu wema na Wazalendo wa Nchi Yao.

Ameeleza kuwa ni lazima kila Mmoja kuwa na dhamira ya Kusimamia Malezi ya Vijana ndani ya familia ili kuwa na Watu wema watakaokuwa Viongozi wa baadae.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewakumbusha Waumini hao Umuhimu wa Kuendelea kuiombea Nchi Amani hasa wakati Huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka Huu.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa bado Serikali inakusudia kutekeleza mambo mengi zaidi ya Maendeleo katika Nyanja tofauti hivyo Suala la kuwepo kwa Amani ndio Kipaumbele Muhimu zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here