Rais Mwinyi: Serikali ya Awamu ya Nane itainua michezo kwa miundombinu ya kisasa

0

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inalenga kufanya mageuzi makubwa ya michezo kwa kujenga na kukarabati viwanja vya kisasa ili kukuza vipaji, kuandaa wataalamu na kuiandaa Zanzibar kushiriki mashindano ya Kimataifa ikiwemo AFCON 2027.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokifungua kiwanja cha kisasa cha Michezo kilichopo Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja Septemba 9, 2025.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema tayari ukarabati wa Amani Complex, Mao Tse Tung na Gombani umekamilika, huku viwanja vipya vikijengwa Kizimkazi (21,000), Fumba (31,000) na viwanja 17 vya mikoa na wilaya.

Halikadhalika, amesisitiza michezo kuwa nyenzo ya kuibua vipaji, ajira, utalii na kudumisha utamaduni, sambamba na ushiriki wa vijana, wanawake na makundi maalum katika mazingira rafiki na salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here