Mambo matatu yatakayofanikisha ushindi wa kimbunga wa Dkt. Samia

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ameelekeza mambo matatu kwa viongozi wa Chama kufanikisha ushindi wa kishindo kwa mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani.

Ameyataja mambo hayo ni kuvunja makundi, kueleza mambo mazuri, makubwa yaliyofanyika katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka minne, kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na kuwashawishi wananchi kuwapigia kura wagombea waliosimamishwa na CCM.

Wasira alieleza hayo mjini Morogoro, alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wakiwemo mabalozi na wenyeviti wa mashina katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Kwa hiyo ndugu zangu baada ya kuwaeleza hayo, nataka niwakumbushe kuvunja makundi na kutangaza kazi zilizofanywa katika miaka minne ya kazi ya mgombea urais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan,”

“Ili watu wakapige kura lazima sisi viongozi tuwahamasishe kwenda kupiga kura, maana kuna wengine wakiwemo wanachama wetu wanasema siamepita Aboud, situmemaliza? Anafikiri kura ya maoni inaweka mbunge.

“Kura ya maoni haijaweka mbunge na ndio maana Aboud tunamwita mbunge mteule tena wa ndani ya CCM kwa sababu wa nje watakuja kuipinga CCM,” alisema.

Aliongeza kuwa “Sasa sisi kazi zetu ni kuhakikisha watu wanajitokeza na tunawashawishi kwa nini waipigie kura CCM, kazi nyingine ni kuwaambia watoke waende wakapige kura.”

Wasira alisema, mabalozi wa nyumba 10 ndio wenye Chama chao kwa kuwa Chama kinaanzia chini na kwamba mabalozolozi wote mwaka huu tumewapa usafiri.

“Kile ni kitendea kazi cha kutoka nyumba hadi nyumba kuwaambia wananchi leo ni siku ya kupiga kurea tokeni nyote mkapige kura.

“Katika mfumo wetu zamani ukikosa mpinzani unapita bila kupingwa, lakini sasa kwa mfano tuna mgombea wetu na wapinzani hawakujitokeza, kule kunataka nguvu zaidi kwa sababu watu watafikiri tayari lakini kumbe yule mgombea ili ashinde lazima kura za ndio ziwe nyingi kuliko hapana, lakini vilevile Rais wa Jamhuri ya Muungano anahitaji kura nyingi kila mahali, sasa atazipata wapi kama watu hawajitokezi kwenda kupiga kura.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here