WAZIRI wa Maji Injinia Kundo Andrea Mathew amepita katika mchujo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya ubunge wa jimbo la Bariadi Mjini.
Mchujo huo umefanyika kwa kufuata taratibu za chama hicho tawala ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu wa Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makala, iliyotolewa leo Julai 29, Injinia Kundo amekuwa mmoja wa watiania wanne ambao wamefanikiwa kupita katika mchujo wa awali kwa Jimbo la Bariadi Mjini.