DC. Magoti aongoza mjadala kuhusu mradi wa Visegese

0

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amefanya kikao cha Wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda.

Magoti akiambatana na Viongozi wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam, walitembelea eneo la Mradi wa upangaji wa upimaji wa eneo la Viwanda Visegese kata ya Kazimzumbwi.

Mradi wa upangaji wa upimaji ulibuniwa kwa ajili ya kutenga Viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo ya Makazi, ulianza kutekelezwa mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291, hivyo eneo hili litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.

Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa.

Katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, Serikali tayari imefikisha huduma ya majina, huku barabara zikiwa mbioni kushughulikiwa ili kupanua wigo wa usafirishaji na kutimiza malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anataka kuwainua wananchi wake kiuchumi na kuboresha maisha yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here