Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amelitaka gazeti la SAUTI YETU kumuomba radhi baada ya kile walichokiandika.
Gazeti la SAUTI YETU toleo la 220 liliandika habari ya DC huyo likiwa na kichwa cha habari ‘DC Nkasi atishia Mwananchi kwa Bastola.’
Baada ya habari hiyo kutoka DC huyo alisema, habari hiyo ilimchafua na kusababisha usumbufu mkubwa kwake.
Kutokana na hilo DC Lijualikali amelitaka Gazeti Hilo kumuomba radhi na kudai fidia ya Bilioni 5.
Aidha, taarifa iliyotolewa na kampuni ya uwakili ya MATWIGA LOW CHAMBERS ambayo DC Nkasi anaitumia, gazeti hilo linatakiwa kuomba radhi ndani ya siku saba.
Baada ya kuomba radhi mteja wao atakuwa na maamuzi ya kumpeleka Mahakamani au la.
Gazeti liliandika taarifa hiyo na kunukuu baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio hilo.
Kwa mujibu wa Gazeti hilo inasemekana tukio hilo lilitokea wilayani Kilombero wakati wa mkesha wa Mwenge.