DAS Mwampamba awataka wazazi kuwapa watoto mlo kamili

0
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amewataka wazazi, walezi wawape watoto vyakula vyenye mchanganyiko wa mlo kamili ili kuwaepusha na changamoto za ukuaji.

Mtela ameyasema hayo akiwa katika kijiji cha Mtepa kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba wakati wa zoezi la Utoaji wa vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Shamba la miti wino lililopo katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Taasisi binafsi na za umma katika halmashauri hiyo vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 39.

Vile vile, Mwampamba alisema wakazi wa Madaba ni watu ambao wanalima na kujishughulisha na shughuli mbali mbali na utajiri wa fedha wanao, lakini tatizo ni namna ya kuzingatia mlo kamili ili kuepukana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Aidha, amewataka wananchi wa Kijiji cha Mtepa kuhakikisha  wanajiunga na Mfuko wa Bima ya afya ili wasipate changamoto ya matibabu pale wanapougua.

Akizungumza katika zoezi hiyo la ugawaji wa vifaa hivyo, Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti wino Groly Kasmir alisema, wametoa vifaa hivyo kwa shule za msingi, makanisa na hospitali kwa lengo la kurejesha kwa jamii, kwa kuwa wakazi hao wapo mstari wa mbele kusimamia hifadhi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here