Abood: Maendeleo aliyoleta Rais Samia Bagamoyo ni ya kupigiwa mfano

0

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

MFANYABIASHARA na Kada wa CCM Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Mohamed Abood Saleh amesema bado ana deni kubwa analodaiwa na wananchi wa Bagamoyo na lazima atalitimiza hata kama asipochukua fomu ya kuwania Ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka huu 2025.

Akizungumza na wanahabari leo Mei 30, 2025, Mjini Bagamoyo, kada huyo alisema kulingana na hatua ya maendeleo iliyoletwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa anaona ni vema akashuka ngazi ya jamii kusaidiana nayo kutafsiri kwa vitendo na kunufaika na maendeleo hayo.

Kada huyo alisema, kuna fursa nyingi katika jamii na wananchi wanatakiwa kuunganisha nguvu na kuzitumia kutokana na kazi kubwa ambayo tayari imefanywa na Serikali ya CCM na hivi sasa Bagamoyo ina maendeleo makubwa tofauti na miaka 10 ya nyuma.

“Kuna baadhi ya ndugu na jamaa walitaka nichukue fomu kuwania Ubunge tena mwaka huu kama nilivyofanya 2020 lakini nasema hapana, nghoja niwasaidie wananchi kutafsiri maendeleo yaliyoletwa na Rais Samia kwa vitendo katika maisha yetu ya kawaida,” alisema.

Alibainisha kuwa, Bagamoyo hivi sasa ina fursa nyingi na imepiga hatua na kimaendeleo makubwa na ni vema wawepo watu kada ya chini ambao watawabainishia kwa vitendo na hicho ndicho kitu ambacho anataka kufanya.

“Maendeleo yanahimizwa na siasa zipo hivyo baadae huko nikiona kuna haja pengine naweza kuwania nafasi hiyo, lakini sio kwa sasa ngoja nilipe deni langu kwa watu wa Bagamoyo ambao wamenilea na kunikuza kwa kusaidiana na jamii kuzitumia fursa zinazoibuka kila siku mjini humo,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here