Wafanyabiashara wakabidhiwa maeneo stendi mpya ya Mlandizi

0

WAFANYABIASHARA wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wamekabidhiwa maeneo ya kufanyia biashara stendi mpya ya Mlandizi iliyopo kata ya Mtambani.

Afisa Biashara Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Ruben Urassa alisema, wafanyabiashara wote waliotuma maombi kwa njia ya maandishi ndiyo waliofanikiwa kupangiwa maeneo kwa haki na usawa bila upendeleo.

Akizungumza kwenye tukio hilo, Urassa aliwataka wafanyabiashara kufuata kanuni, sheria na mkataba ulioandikwa baina ya halmashauri na wafanyabiashara.

Hivyo, ametoa rai kwa watakaokiuka mkataba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here