MGOMBEA wa Urais kupitia CCM Zanzibar, ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ijayo itaweka kipaumbele kwenye ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula na matangi ya mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha uhakika na kudhibiti mfumuko wa bei.
👉 Serikali itanunua mazao ya wakulima wakati wa mavuno, kutoa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu, kuimarisha umwagiliaji na kuhakikisha soko la uhakika.

👉 Dkt. Mwinyi amesema pia Serikali itajenga matangi makubwa ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na changamoto za bei za kimataifa.
👉 Uchumi wa Zanzibar umeimarika kutoka 4% mwaka 2020 hadi 7% mwaka 2024, Serikali imechukua hatua kwa kuongeza mishahara, pensheni na posho.

👉 Vipaumbele vingine ni pamoja na kuimarisha huduma za bandari, utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, na kuongeza thamani ya zao la mwani ambalo ni tegemeo la akinamama wengi Zanzibar .
Akihitimisha, Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, huku akiahidi kampeni safi na za kistaarabu kupitia CCM.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 12, 2025, alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea muelekeo wa Serikali ijayo katika hoteli ya Golden Tulip, Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.