Mlandizi, Gwata wang’ara kwa huduma bora

0

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Erasto Makala, ametoa pongezi kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi pamoja na Zahanati ya Gwata kwa kutunukiwa vyeti vya ubora wa utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Pwani.

Vyeti hivyo vimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa vituo hivyo katika kuboresha afya za wananchi kupitia huduma bora, zenye tija na zinazozingatia utu wa mgonjwa.

Katika hatua nyingine, Makala amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kutunukiwa cheti maalum na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kutokana na juhudi zake za kuwawezesha Maafisa Maendeleo ya Jamii kushiriki kwa wingi kwenye kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here