MENEJA wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Tanga, Julius Temba (pichani – wa pili kutoka kushoto- mbele) amemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Mark Kihulla katika dua maalum ya kumwombea marehemu Mzee Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dua hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Sharriff Haidar Wakfu na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa Serikali na wananchi mbalimbali.
Marehemu Hafidh Ameir Hassan alifariki Septemba 7, 2026.
Akizungumza na MBIU YA VIPIMO kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa WMA, Temba ametoa pole kwa Mheshimiwa Rais na familia nzima na kuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.