Wanaoshiriki UMISSETA 2024 wahakikishiwa usalama

0

MKUU wa Mkoa wa Tabora Paul Matiko Chacha, amewahakikishia Usalama wanamichezo na wageni waliopo Tabora kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya UMISSETA 2024.

Ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye Mashindano hayo ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania, yanayofanyika Mkoani Tabora kwa mara ya tatu mfulululizo.

“Tuna wanamichezo zaidi ya Elfu tatu na waalimu zaidi ya mia saba, hii ni idadi kubwa lakini hadi kufikia sasa wote wapo salama na mkoa kwa ujumla uko salama” alisisitiza RC Chacha.

Kuhusu maazimio ambayo yametolewa na viongozi mbalimbali juu ya kukuza michezo, amesema kuwa Mkoa utayasimamia yote yaliyoazimiwa kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.

Akitoa salam za Mkoa kwa Mgeni rasmi Waziri wa Sanaa utamaduni na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro, Mkuu huyo wa Mkoa amemhakikishia kuwa wamejipanga kahakikisha kuwa michezo inapewa kipaombele katika shule mbalimbali.

“Viongozi wetu wa kitaifa akiwepo Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024 alisisitiza juu ya kukuza na kuendeleza vipaji vitakavyoibuliwa katika mashindano haya, na sisi kama mkoa tumejipanga kutekeleza hilo” alisema Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here