MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Uzairu Abdul Athumani leo Desemba 24, 2025 ametoa maneno ya Baraka kwa Bondia Hamadi Furahisha kama Mwakilishi wa Tanzania katika Pambano la Ngumi dhidi ya Bondia Hanock Phiri kutoka Malawi linalotarajiwa kufanyika Ijumaa Desemba 26, 2025 eneo la Ware House, Masaki Jijini Dar es Salaam.
Uzairu amehimiza uungwaji mkono wa Mabondia wa ngumi akisisitiza kuwa kwa sasa ngumi si mchezo tu bali ni fursa ya Ajira kwa Vijana wa Tanzania ambapo pia kwa upande wake ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Wanamichezo wote.
‘’Tuwaunge Mkono Vijana wa Michezo, Michezo ni Ajira na Temeke tupo vizuri kwenye michezo nenda kaiwakilishe Tanzania,” alisema Uzairu.
Kwa upande wake Bondia Hamadi Furahisha ametoa shukrani kwa fursa na heshima hiyo na kuahidi kupambana kwa nguvu zote kuiletea heshima Tanzania katika medani za Ndondi Kimataifa.
‘’Nimekuja kuchukua baraka kwa Mstahiki Meya , nashukuru sana kwa nafasi hii na naahidi kuleta ushindi,” alisema Bondia Hamadi.