WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed amewataka wanahabari na maafisa Habari kulinda maadili, misingi na mipaka ya taarifa za watu binafsi ili kuepusha migogoro katika jamii.
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kinazini katika ufunguzi wa mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa maafisa,wanahabari na wahariri wa vyombo vya habari
Alisema, uwelewa wa Ulinzi wa taarifa binafsi ni jambo muhimu kwani inaweza kuhifadhi na kulinda taarifa hizo pamoja na kujikinga uchochezi unaopelekea kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Dkt. Khalid alisema, kutokana na ukuaji wa teknolojia, ni rahisi kusambaza na kuingilia faragha ya mtu, jambo ambalo linahatarisha usalama wa taarifa binafsi. “Tunatakiwa tuwe waangalifu kwa kila jambo.”
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Emanuel Lamic Mkilia alisema, wanahabari wana jukumu la kulinda taarifa binafsi za watu ili kuepuka madhara yanayoweza kukitokeza
Alisema, Sheria ya mwaka 2022 inatilia mkazo suala la matumizi ya faragha ya mtu, kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria kwani taarifa binafsi ni haki ya kila mtu ni vyema kuheshimiwa na kulindwa
Aidha, amefahamisha kuwa kwa Dunia ya Sasa taarifa zinaweza kutimiza vibaya ikiwemo madhara ya wizi wa kifedha hivyo mafunzo hayo yatajadili mbinu Bora za kuhakikisha Ulinzi wa taarifa za watu
Akiwasilisha mada ya Misingi ya Ufatiliaji Mkurugenzi wa Usajili na uzingatiaji Eng. Stephen Wangwa alisema, msingi wa mtunza taarifa lazima zilindwe wakati wote na kuweka taarifa sahihi ambazo zinaendana na wakati
Nao washiriki waliyopatiwa mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi yale walivyopatiwa ili kuepusha madhara kwa wananchi
Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha Maafisa Habari kutoka taasisi za Serikali na waandishi mbalimbali na mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo masuala ya Ulinzi wa mtu binafsi ambapo Kaulimbiu ni “Faragha yako ni wajibu wetu.”