UCSAF yaendelea kutoa elimu kwa wananchi Nane Nane Dodoma

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda lao katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwemo ujenzi wa minara ya mawasiliano.

Kwa kushiriki maonesho ya Nane Nane, UCSAF inaendeleza dhamira yake ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kunufaika na mawasiliano bora kama chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

UCSAF inapatikana ndani ya banda kuu la Government Zone – Pavilion 4, ambapo wananchi wote wanakaribishwa kutembelea na kupata huduma mbalimbali pamoja na maelezo kuhusu juhudi za Serikali katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika kwa wananchi wote, hasa maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here