Uchumi wa buluu ni dhana inayochagiza ukuaji wa uchumi – Masauni

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesemea Uchumi wa Buluu ni dhana inayochagiza ukuaji wa uchumi kupitia matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira na ushirikishwaji wa jamii.

Alisema mesema hayo wakati wa kikao cha Mawaziri cha kuwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini kwa mwaka 2024/25 na 2025/26 kilichofanyika Dodoma Februari 13, 2025.

“Shughuli za Uchumi wa Buluu hapa nchini zinatekelezwa kwa sera, sheria, miongozo, mikakati na mipango ya kisekta ikiwemo, Uvuvi, Nishati, Uchukuzi, Maliasili na Utalii, Maji, Umwagiliaji, Viwanda na Biashara, Uhifadhi wa Mazingira, Madini, na Uwekezaji.

“Pamoja na uwepo wa sera na sheria hizo, kumekuwepo na changamoto mtambuka zinazochangia Taifa kutonufaika ipasavyo na rasilimali za Uchumi wa Buluu zikiwemo kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu, Kukosekana kwa Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji, Uwekezaji usio wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu na Uhaba wa utafiti na ujuzi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu.

Alisema, kwa kuzingatia changamoto hizo na ili kufanikisha azma ya Serikali katika kutumia rasilimali za Uchumi wa Buluu na kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu, Serikali iliaandaa na kupitisha Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 na Mkakati wake wa utekelezaji wa mwaka (2024-2034) iliyozinduliwa Juni 5, 2024.

Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 imezingatia maeneo muhimu ambayo ni Uratibu wa Shughuli za Uchumi wa Buluu ili kuwa na mfumo jumuishi wa uratibu miongoni mwa wadau wanaosimamia na kutekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu nchini, Matumizi ya Maeneo ya Maji ili kuwezesha nchi kunufaika ipasavyo na fursa za Uchumi wa Buluu kwa kuzingatia mahitaji ya shughuli za kiuchumi, kijamii na uhifadhi wa mifumo ikolojia na mazingira na Usimamizi katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu ili kuimarisha uratibu wa rasilimali zote za Uchumi wa Buluu katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here