Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema, vyama vyote vya siasa vina uhusiano mzuri na chama hicho na sio kama inavyodaiwa na ACT Wazalendo.
Akizungumza Mjini Zanzibar, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema CCM kina uhusiano mzuri na vyama vyote kikiwemo ACT Wazalendo.
Alisema, Mwenezi huyo kuwa, yeye binafsi ameshiriki shughuli mbili ambazo CCM walialikwa na kushika kibendera cha ACT Wazalendo.
Mbeto anautaja uzinduzi wa Kampeni ya Ahadi za Chama ‘Brand Of Promise’ na Maalim Seif Sharrif Hamad Foundition ni kati ya shughuli za ACT alizokwenda kukiwakilisha chama.
“Sheria ya msajili inasema vyama vyote ni vya waTanzania, walitualika tukaenda hivyo sio kwamba tuna uhusiano na Ada Tadea, Chauma au NRA tu hata ACT tuna mahusiano mazuri na vyama vyote,” alisema.
Mbeto alihoji kilipo chama kinachouzwa kama wanavyodai ACT Wazalendo na kubainisha kuwa hizo ni propaganda na kuishiwa hoja.
“Hawana la kusema zaidi ya kuhubiri ubaguzi na kusahau kuwa Zanzibar ni kisiwa chenye watu mchanganyiko wa Mataifa yote.