TARURA kuanza kutangaza zabuni za mwaka 2025/2026

0

📌Barabara zenye changamoto kufikiwa

📌Zipo barabara zenye kipaumbele kwa jamii

Singida

MTENDAJI Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewaagiza Mameneja wa Mikoa nchi nzima kuanza kutangaza zabuni za mwaka wa fedha 2025/26.

Mhandisi Seff ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida pamoja na kuzungumza na Mameneja wa TARURA wa wilaya katika mkoa huo.

Alisema, katika zabuni hizo zizingatie barabara zenye kipaumbele kwa wananchi na zile zenye changamoto za kupitika

Pia, Mtendaji Mkuu huyo aliwasisitiza Mameneja kufanya matengenezo ya barabara kwa wakati na kuhakikisha miradi yote ya kwenye maeneo yao inaanza mapema.

Aidha, amewataka Mameneja wa wilaya kuandaa mipango ya kuboresha barabara kwa kuzingatia vipaumbele.

Mhandisi Seff yupo Mkoani Singida ambapo jana Mei 1, 2025 alishiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani na kupewa zawadi ya fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Mfanyakazi hodari wa TARURA kwa mwaka 2024/25.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here