MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI amesema Soko jipya la Kariakoo ni kielelezo cha Taifa Kimataifa kwani litakuwa kujihudumia Mataifa mengi zaidi.
Nyamoga ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa soko hilo la Kimataifa la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
“Hili soko ni kielelezo cha Taifa kimataifa na Kamati unashauri siku ya ufunguzi wa soko hili mataifa ambayo ni wanafaika wa soko hili pia waalikwe” alisisitiza.
Alisema, Mataifa ambayo ni wanufaika soko hili kubwa la kimataifa ni pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Zambia na mataifa mbali mbali yanayozunguka Nchi yetu.
Aidha, Nyamoga ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi wake wa kufanya soko la Kariakoo kufanyakazi usiku na mchana kwani itaongeza chachu ya maendeleo katika Taifa letu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange alisema soko la Kariakoo ni Taswira ya Taifa kwani ni Soko kubwa zaidi katika Nchi hivyo wasimamizi wanatakiwa kuzingatia usafi wa soko hilo kwa maslahi mapana Zaidi ya Taifa.
Aidha, Dkt. Dugange ameipongeza timu zima ya usimamizi wa soko hilo wa kufanikisha ujenzi wa huu wenye hadhi ya Kimataifa.