Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ni miongoni mwa mamia ya washiriki katika mbio za NMB zilizofanyika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam.
Kauli mbiu katika mbio hizi ilikuwa ‘Mwendo wa Upendo’ zilizolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Fistula kwa wanawake wenye tatizo hilo kupitia CCBRT.
Mgeni rasmi katika mbio hizo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ambapo amefanikisha kuchangishwa kwa Shilingi Milioni 600 kwa ajili matibabu ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.