WAZIRI wa Fedha Mwigulu Nchemba, ametangaza bungeni kuwa Serikali imefuta kodi kwenye matangazo yote ya magazeti yanayozalishwa nchini.
Dkt. Nchemba alitoa taarifa hiyo wakati akisoma Bajeti Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2025 / 2026 jana.
“Hatua hii itatoa ahueni kubwa kwani kati ya chanzo cha kifo cha magazeti imekuwa hii Kodi ya VAT.
“Imekuwa kila mara unatoa risiti ya EFD kwa matangazo, halafu hiyo risiti inachelewa kulipwa, tunadaiwa VAT ambayo hatujapokea malipo,” alisema Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).