SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilikabidhi kompyuta 20 za mezani pamoja na vifaa vingine vya TEHAMA katika Shule ya Msingi Samia Suluhu Hassan iliyopo kijiji cha Msomera, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Kupitia mradi huu, UCSAF imefanikiwa kufikisha vifaa vya TEHAMA katika shule 1,121, nchini ambapo kwa wastani kila shule kupatiwa kompyuta 5, projekta 1 na printer 1.

Lengo ni kuhamasisha na kukuza uelewa wa TEHAMA miongoni mwa wanafunzi, ili waweze kutumia teknolojia kwa ufanisi katika kujifunza na kujiandaa na fursa za Kidijitali wanapofikia vyuo vikuu au soko la ajira.
Hadi kufikia Desemba 2024, Serikali kupitia UCSAF ilikuwa imefikisha vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.94, na utekelezaji wa awamu zinazofuata unaendelea kwa lengo la kuhakikisha shule zote nchini zinapata fursa sawa za TEHAMA.
