NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa taa za barabarani kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 katika miji ili kuongeza usalama na muda wa kufanya kazi
Akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, Mhandisi Kasekenya amesema mradi huo utaanza kufanyika mwaka wa fedha 2026/2027 baada ya bajeti kupitishwa na Serikali imetoa kipaumbele maalum kwa mikoa ya Dar es salaam na Arusha kutokana na uwepo wa mashindano ya Afcon na barabara zitakazotumika
“Serikali inatambua umuhimu wa taa za barabarani hadi sasa taa 426 zimefungwa kwenye barabara za halmashauri ya Chato zinazohudumiwa na TANROADS “,amesema Mhandisi
Aidha Mhandisi Kasekenya amesema Serikali imeshapata orodha ya miji yote inayohitaji kufungwa taa na kusisitiza maeneo yote muhimu ajili ya kuongoza magari na kuimarisha usalama kwa wananchi wanaotembea kwa miguu
Naibu Waziri amesema Serikali imetenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuweka taa kwenye miradi yote inayoendelea kujengwa katika miji,pia kusimamia na kufuatilia uwekaji wa taa ili kupendezesha miji hiyo na kuondoa adha kwa wafanya biashara nyakati za usiku.