Samia Housing II – Kijichi yazidi kusonga mbele kwa kasi

0

MENEJA wa Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, amefanya ziara fupi kwenye mradi wa Samia Housing II – Kijichi kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi yanayoendelea.

Katika ziara hiyo, Saguya alishuhudia hatua mbalimbali za ujenzi zinazofanyika likiwemo kumwaga blinding katika block E, kuandaa level za blinding block D, kurekebisha level block C, pamoja na uchimbaji wa msingi katika block A.

Aidha, aliona maandalizi ya sehemu ya kuwekea tanki la maji yanayoendelea kujengwa, hatua muhimu inayolenga kuhakikisha wakazi wa baadaye wanapata huduma ya maji kwa uhakika.

Vilevile, timu ya wahandisi na mafundi wa NHC imekamilisha setting out za pad blinding block B na kuanza uchimbaji maalum wa deeper pads kwenye eneo hilo.

Sambamba na kazi hizi, usafi wa jumla umefanyika ili kuhakikisha eneo lote la mradi linabaki safi na salama kwa shughuli za ujenzi.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Meneja Saguya alisema NHC inaendelea kusimamia mradi huu kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha nyumba zinakamilika kwa viwango bora na ndani ya muda uliopangwa.

“Lengo letu ni kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora, salama na yenye huduma muhimu,” alisema.

Mradi wa Samia Housing II – Kijichi ni sehemu ya mkakati wa Serikali kupitia NHC wa kuongeza upatikanaji wa makazi bora jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotafuta nyumba za kisasa na zenye miundombinu ya kisasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here