Rais Samia kuzindua bandari kavu ya Kwala

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani, pamoja na miradi mingine mikubwa ya kimkakati, Julai 31, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo kubwa la kihistoria.

Katika ziara hiyo, Rais atazindua safari rasmi za Treni ya Mizigo kwa njia ya Reli ya Kisasa (SGR), kupokea mabehewa ya mizigo kwa njia ya Reli ya Zamani (MGR), pamoja na kuzindua Kongani ya Viwanda ya Kwala yenye jumla ya viwanda 250 vinavyotarajiwa kujengwa, ambapo viwanda saba tayari vimeanza uzalishaji.

Bandari Kavu ya Kwala ina uwezo wa kuhudumia zaidi ya makasha 300,000 kwa mwaka, hatua inayotarajiwa kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam kwa takribani asilimia 30.

Aidha, jumla ya mabehewa 160 ya mizigo yanatarajiwa kupokelewa, yakiwemo mapya, yaliyokarabatiwa na yaliyotolewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).

Miradi hiyo inaakisi dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha miundombinu ya reli, bandari, na viwanda kwa lengo la kuongeza ushindani wa kikanda na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchukuzi na biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here