RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Mamia ya Wana Mazoezi Katika Matembezi ya Tamasha la Siku ya Mazoezi Kitaifa Kisiwani Pemba.
Matembezi hayo ya Kilomita Tano yalioanzia Kinyasini hadi Uwanja wa Mnazi Mmoja Wete yaliambatana na Mazoezi ya Viungo.
Akizungumza baada ya Kushiriki Mazoezi hayo Rais Dkt. Mwinyi amewasisitiza Wananchi kuendelea kufanya Mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuepuka Maradhi yasiyoambukiza.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Maradhi yasioambukiza ikiwemo Kisukari, Presha, Unene uliopitiliza Shinikizo la Moyo yamekuwa Tishio la Kiafya hivi sasa, lakini yanaepukika kwa jamii kufanya mazoezi.
Rais Dkt. Mwinyi amekihakikishia Chama Cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (Zabesa) kuwa Serikali itaendelea Kuunga Mkono Tamasha hilo na kukipongeza Chama Cha hicho kwa kuliendeleza Tamasha hilo kwa Mafanikio kwa Miaka 15 na kusisitiza kuwashawishi Watu wengi zaidi kufanya Mazoezi.
Akizungumzia Suala la Amani Rais Dkt. Mwinyi amewaasa Viongozi wa Dini na Wanasiasa kuhubiri Amani kwa wananchi na kuacha kuhubiri Chuki, Fitna na Mifarakano ya Kisiasa wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu.