RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya kauli na matendo ya uchochezi yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, akisisitiza kuwa taifa lisilo na amani hupoteza kila kitu.

Akizungumza baada ya kufungua Msikiti wa Jammah, Bwejuu – Mkoa wa Kusini Unguja leo Septemba 5, 2025, Dkt. Mwinyi amewahimiza wafadhili na waumini kuwawezesha maimamu na walimu wa madrasa ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Aidha, aliwashukuru waumini na mfadhili wa msikiti huo kwa ukarabati na ujenzi wa ghorofa moja.
