Rais Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka China

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka China kuwekeza nchini hususan kuendeleza sekta ya afya na tafiti za dawa za asili nchini.

Rias Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Timu ya Wataalamu kutoka Chuo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha China waliofika Ikulu kuonana naye.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alisema Zanzibar imeendelea kuthamini mchango na misaada ya China kwa Zanzibar katika sekta tofauti za Maendeleo na Kijamii iliyodumu kwa muda mrefu tangu na baada ya Mapinduzi na kuendelea hadi sasa.

Halikadhalika, ameeleza kufarijika na misaada katika Sekta ya Afya inayotolewa na timu za Madaktari Bingwa wanaokuja nchini kwa nyakati tofauti kutoa matibabu kwa Jamii, Dawa na huduma katika Hospitali na vituo vya afya na mafunzo kwa watendaji wa Sekta ya Afyanchini.

Naye Kiongozi wa Ujumbe huo Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha China Professa Song Li Jwan alisema Ziara yao Zanzibar imelenga kuimarisha ushirikiano baina ya China na Zanzibar hususan katika Maendeleo ya Sekta ya Afya na kuendeleza Tafiti za dawa za Asili baina ya pande hizo mbili.

Amebainisha kuwa hatua hiyo ni Utekelezaji wa Sera ya kitaifa ya China kwa Nchi za Afrika ikiwa ni utekelezaji wa Malengo ya Mkutano wa Beijing wa mwaka 2024 uliojikita katika Uimarishaji wa Sekta ya Afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here