Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na uongozi wa Kampuni ya Miss World, ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake, Julia Evelyn Morley, pamoja na Mshindi wa Miss World 2025, Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, na Miss World Africa, Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Zanzibar, Julai 21, 2025, ambapo pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii Zanzibar.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Aboud Jumbe; Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Amina Hassan Ameir na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Arif Abbas Manji.