Rais Dkt. Mwinyi ajivunia utendaji wa SMZ

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi kimesema kina matumaini makubwa ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, baada ya kutekeleza ahadi zake za kisera zilizoleta maendeleo na kuwatumikia wananchi kwa Haki na Usawa.

Kimesisitiza kitashinda tena na kuongoza Serikali ya zanzibar kwa ridhaa na matakwa ya wananchi ili kukata ngebe za upinzani Visiwani humu.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa SMZ , Dk Hussein Ali Mwinyi, ameeleza hayo katika mkutano wa hadhara akifungua Tawi la CCM la kisasa huko Mpendae Juu, Mkoa wa Mjini Magharibi Kisiwani Unguja.

Rais Dkt Mwinyi alisema CCM kitashinda kwa kishindo na kupata kura nyingi bada ya kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi kwa vitendo, hali iliyoleta mabadiliko ya kimaendekeo.

Alisema, kutokana na CCM kutimiza ahadi zake zilizoleta mageuzi katika sekta muhimu za maendeleo ,hatua hizo zimekuza ustawi kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM Mwaka 2020/2025.

“Wananchi na wana CCM wa Mkoa wa Mjini Magharibi nina furaha kuona mmejiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Kazi iliobaki na jukumu lenu ni kupiga kura ifikapo oktoba mwaka huu,” alisema Rais Dkt. Mwinyi.

Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alisema, “kujitokeza kwenu na kupiga kura kwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, Wabunge , Wawakilishi na Madiwani wa chama chenu kutakata ngebe za wapinzani wetu.”

Aliwasisitiza wananchi na wana CCM, kwamba kazi kubwa iliyobaki iko mikononi mwao kujitokeza mapema na kupiga kura “Kazi imebaki kwenu ya kukirudisha chama chenu madarakani. Tutahakikisha Zanzibar inazidi kupaa kimaendeleo kuliko ya miaka mitano ya kwanza. Hiyo ni ahadi yangu kwenu na kwa wazanzibari wote.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here