Naibu Waziri Kapinga agawa majiko banifu 1500 Msomela

0

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amekabidhi majiko banifu pamoja na majiko ya gesi kwa wakazi wa Kijiji cha Msomela, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Serikali za kuhakikisha ifikapo 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Katika hafla hiyo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umetoa majiko banifu 1500 yenye gharama ya Shilingi Milioni 82.5 ikiwa ni muendelezo wake katika kufanikisha azma hiyo ya Serikali yenye lengo la kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Akishukuru msaada huo Naibu Waziri wa Nishati Kapinga alisema, Taifa Gas walichokifanya Msomera ni kupanda mbegu ya Mabalozi wa kudumu ambao watakuwa na wataendelea kuwa wateja wao.”Imarisheni huduma hii hapa Msomelana jirani kuzunguka Msomela ili wananchi hawa gesiikiisha wasipate tabu mahala pa kwenda kubadilisha,”

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Davis Deogratius alisema, timu yake tayari imeshafanya mchakato wa kuwa na mawakala hapo Msomela tena wazawa, hivyo wasiwe na wasiwasi kwani gesi ikiwaishia wataipata Msomela na wale ambao hawajabahatika kupata mitungi ya Taifa Gas tayari ipo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando amewashukuru Taifa Gas kwa msaada mkubwa kwa Wananchi wake wa Msomela na aliendelea kuwaomba kuwa wananchi wake ni wengi hapa watapata nusu yao tu na nusu bado hivyo wakipata nafasi tena wasiwasahau Wananchi wa Msomela waliokosa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here