Mtendaji Mkuu UCSAF atembelea mabanda ya taasisi za Serikali Nanenane Dodoma

0

MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda, ametembelea baadhi ya mabanda ya taasisi za Serikali yanayoshiriki katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Mhandisi Mwasalyanda alitembelea banda la Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo alipata maelezo na elimu kuhusu huduma na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara hiyo, hususan katika maeneo ya TEHAMA, miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma jumuishi kwa wananchi.

Pia, alitembelea mabanda ya taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo, zikiwemo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Katika kila banda, alijionea huduma zinazotolewa na kujadili kwa kina namna taasisi hizo zinavyoweza kuendelea kushirikiana na UCSAF katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na maendeleo ya kijamii, hasa kwa wananchi wa maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi.

Ushiriki wa UCSAF na taasisi nyingine katika maonesho haya ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwasogezea wananchi huduma muhimu na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari kama msingi wa uchumi wa kidijitali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here