Msikwepe majukumu yenu, wahudumieni wananchi

0
MKUU wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili.

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutokwepa majukumu yao katika kuwahudumia wananchi.

Hayo ameyabainisha Mjini Singida alipokuwa akifungua Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Watendaji wa Kata na Tarafa wa Mkoa wa Singida kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Alisema, wapo baadhi ya maafisa hao hukwepa majukumu yao kwa kuchagua kazi za kufanya na wakati mwingine kutoa lawama kwa Serikali kuona kazi nyingine hapaswi kutekeleza wao.

“Mnajisahau kuwa nyie ndio Serikali wa eneo husika mnalifanyia kazi mnapaswa kushughulikia kila sekta kama elimu, miundombinu, afya, kilimo,uvuvi, amani, usalama, michezo na maafa yote haya mnapaswa kushughulika nayo,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais- TAMISEMI Hamisi Mkunga amewakumbusha maafisa hao kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliofundishwa kwa kuwa mada zilizofundishwa zinaendan sambamba na utekelezaji wa majukumu yao.

“Hakutakuwa na kisingizio cha kutokufanya kazi kwa sababu ya kutokujua sheria, taratibu na kanuni vyote hivyo wamefundishwa, mafunzo haya mliopatiwa mkatekeleze kwa vitendo tutawapima,” alisisitiza Mkunga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here