Mradi wa Julius Nyerere kupunguza Tani Milioni 3 za gesijoto

0

MRADI wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere umetajwa kuwa na uwezo wa kupunguza tani Milioni 3 za gesijoto kwa mwaka, kati ya tani 138 hadi 155 zinazoweza kupunguzwa kupitia shughuli mbalimbali nchini kwa mwaka.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Hamad Yussuf Masauni amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26, bungeni jijini Dodoma Juni 23, 2025.

Alisema, pamoja na mradi huo wa kimkakati wa kuzalisha umeme uliopo Rufiji mkoani Pwani, Tanzania inatajwa kuwa ni chujio la gesijoto kupitia miradi mingine ikiwemo ya Reli ya kisasa (SGR), Mabasi yaendayo Haraka (DART), misitu, taka, mikoko iliyopo kwenye fukwe.

Akiendelea kuchangia hotuba hiyo, Masauni alisema mabadiliko ya tabianchi yana athari kubwa kwa Tanzania na dunia kwa ujumla na kusababisha hali ya hewa isiyotabirika, ukame, mito kukauka na hivyo kuathiri uzalishaji wa nishati ya umeme na kilimo.

“Kutokutabirika kwa hali ya hewa kumeleta athari za mafuriko na kuathiri uchumi, miundombiunu kuharibika ikiwemo fukwe ambazo ni sehemu ya utalii, hivyo sisi kama taifa tunapaswa kuungana na mataifa katika kutatua changamoto hii,” alisisitiza.

Aidha, Mhandisi Masauni changamoto ya gesijoto ni fursa kubwa ambayo nchi inaweza kuitumia na kufaidika nayo, hivyo kuchangia kwa kiasi kikukbwa katika maendeleo ya kiuchumi hususan biashara ya kaboni.

Alisema, mabadiliko ya sheria ya mazingira yaliyofanyika yakitaka miradi yote izingatie mabadiliko ya tabianchi sanjari na hatua ya kulifanya Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kuwa Mamlaka kamili ili kuhakikisha wanazingatia sheria.

Halikadhalika, Masauni alisema kutambuliwa kisheria kwa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kuchangia Tanzania kupata mialiko na kusaini makubaliano ya ushirikiano wa biashara ya kaboni nchini Japan, Norway na Denmark na kuiwezesha nchi kupata masoko ya biashara hiyo.

Kutokana na hatua hiyo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi katika sekta ya mazingira ambayo yameleta mafanikio makubwa hasa katika kuingiza fedha kupitia mifuko mbalimbali ikiwemo GEF na AF.

Halikadhalika, Waziri Masauni alipongeza Wizara ya Fedha kwa hotuba ya bajeti ambayo inaakisi matumizi ya nishati safi ikiwemo kuondoa kodi ya ongezeko la thamani katika gesi za magari hatua itakayosaidia kupungua matumizi ya mafuta kwa vyombo hivyo vya moto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here