MINARA hiyo imeanza kutoa huduma za simu na intaneti, jambo linaloongeza upatikanaji wa mawasiliano katika vijiji na maeneo ya pembezoni yaliyokuwa na changamoto za mawasiliano.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za kidijitali ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Minara iliyosalia ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, na kukamilika kwake kutahakikisha lengo la Serikali la kufikisha huduma za mawasiliano bora na za uhakika kwa Watanzania wote.