Mbeto: Majina zaidi ya matatu wagombea CCM ni uamuzi wa vikao

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

UAMUZI wa kuongeza majina ya watakaopigiwa kura za maoni CCM kutoka matatu ya sasa hadi zaidi kwa wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani itagemea maamuzi ya vikao vya mchujo, vinavyotarajiwa kuanza rasmi Julai 3, mwaka huu 2025.

Akizungumza na wanahabari, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema, suala la kuongeza idadi ya watakaopigiwa kura za maoni itategemea vikao vya mchujo.

Mbeto alisema, ni kweli makada wengi wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama na kakuni haielekeze idadi ya majina yatakayorudi isipokuwa vikao viliamua yawe matatu.

“Unajua CCM sio mtu ni chama hivyo kama hilo litajitokeza, likajadiliwa na ikaonekana inafaa kuongeza majina ya mchujo, maelekezo yatatolewa,” alisema Mbeto na kubainisha kuwa chama ni kikubwa nani sikivu.

Alisema, kutokana na hamasa iliyoonyeshwa na makada wa chama hicho ni kweli inawezekana wakapatikana wanachama 20 hadi 50 na wote wana sifa zinazohitajika, hivyo pengine hilo linaweza kujitokeza na hatua zikachukuliwa.

Mwenezi huyo anabainisha kuwa, kazi ya kwanza ya vikao ni kujua idadi ya waombaji katika nafasi zote na majina yakirudi na kupigiwa kura, vikao vitakaa kwa uamuzi wa mwisho kabla hayajapelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here