Mbeto: Hotuba ya Rais Mwinyi akifunga Baraza la Wawakilishi Z’bar ni ya kimapinduzi

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hotuba ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kabla ya kuahirisha kulivunja kuvunja Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) ni ya kujivunia ufanisi wa sera na mkakati wa maendeleo ya kimapinduzi.

Chama hicho pia kimeitaja hotuba hiyo licha ya kugusa sekta muhimu na utendaji wa kazi za Serikali, imeonyesha kupanda grafu ya maendeleo katika sekta za umma na binafsi, Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, amesema licha SMZ kufanya mageuzi ya kimapinduzi, Serikali kwa miaka mitano iliyopita, imeleta tija kwa maendeleo yaliyofikiwa.

Mbeto alisema, utekelezaji wa kisera 2020-2025, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejiegemeza zaidi katika kukuza sekta za utalii, viwanda, kilimo na michezo na kasi ya ukuaji Uchumi wa Bluu, pato la mtu na Taifa kwa ujumla.

Alisema, kwa miaka mitano iliyopita, SMZ chini ya Rais Dkt. Mwinyi, imefanikisha malengo ya kisera katika sekta za elimu, uwekezaji, viwanda, afya, kilimo, maji, uvuvi na biashara.

“Pia ajira, usafiri wa anga na tumefanikiwa kugawa vitalu kwa makampuni ya uchimbaji wa gesi na mafuta,” alisema Mwenezi Mbeto.

Alibainisha kuwa, hotuba ya Rais Dkt. Mwinyi imewafumbua macho na masikio wanasiasa wenye hulka ya ujuvi na ukaidi. Kila mtu amesikia mambo yaliofanikishwa na SMZ kwa miaka mitano iliopita.

Aidha, hotuba hiyo imetaja hatua zilizochukukiwa kimkakati lakini pia kuelezea matarajio na kufikia malengo mahususi kwa miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 .

“CCM imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na mkakati wa utendaji na utekelezaji wa kisera chini ya Awamu ya Nane. Chama kina imani kubwa na uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi na watendaji wa Serikali yake.” alisisitiza Mbeto

Pia, Katibu huyo Mwenezi, alisema CCM kimefurahishwa kwa hatua madhubuti za SMZ za kuendeleza Umoja wa Kitaifa, kupinga ubaguzi wa aina yoyote na kutilia mkazo dhima ya kuwaunganisha wananchi.

Mbeto alisema, ni aibu kubwa kwa wanasiasa ambao mara kadhaa, wamekuwa wakipotosha ukweli wa mambo na kudai hakuna kilichofanywa na SMZ kwa miaka mitano iliyopita.

“Yote yalioahidiwa kisera na Rais Dkt. Mwinyi wakati wa kampeni za mwaka 2020 ametimiza ahadi zake. Ni kawaida ya CCM kuahidi na kutekeleza kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025,” alisema.

Mbeto alisema, kutokana na kupatikana na ufanisi wa kisera uliyofanyika miaka mitano iliyopita, CCM ina hakika ya kushinda tena Uchaguzi Mkuu Zanzibar, ifikapo Oktoba mwaka huu 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here