Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MAPOKEZI Makubwa aliyopata Naibu Katibu Mkuu (CCM) Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi Visiwani Pemba, hotuba zake kwa viongozi, wanachama wa chama chake na wananchi kwa ujumla vinaonyesha jinsi gani chama hicho kilivyo na hazina kubwa ya viongozi tofauti na vyama vingine vya siasa nchini.
Akizungumza na wanahabari Ofisi Kuu, CCM Kisiwandui kuhusiana na tathmini ya ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi na Uenezi, Komredi Khamis Mbeto Khamis amesema chama chake kina hazina kubwa ya viongozi wenye uzalendo walio tayari kulitumikia Taifa lao.
Mwenezi huyo alisema, Mwenezi Abdi ambaye ni zao la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ambako pia amefanya mambo makubwa na ni hazina mojawapo ambayo anabainisha kuwa, jina lake Julai 29, 2026, lilipowasilishwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu (CCM) Taifa, kilichofanyika Ikulu Ndogo Tunguu, lilipitishwa na kuidhinishwa.
Komredi Mbeto alisema, anamjua Abdi kabla lakini utendaji wake akiwa UVCCM ndio uliofanya akaonwa Ofisi Kuu Kisiwandui, akalelewa na mtangulizi wake kwenye nafasi hiyo, Dkt. Mohammed Saidi Dimwa na hivi sasa anapomkabidhi mikoba, chama kinamridhia kuitumikia nafasi hiyo akibainisha kuwa Rais Dkt. Mwinyi kaongezwa ‘jembe’ la kuwatumikia wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, siku alipokwenda Ikulu kujitambulisha na kukabidhiwa majukumu, alisema hana shaka na utendaji wa Abdi.
“Nina ana imani na uwezo wake nikizingatia uzoefu na utendaji aliouonyesha akiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar akachape kazi kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi na watendaji wa chama na kuendelea kuwatumikia wananchi kwa weledi na uadilifu,” aliandika Rais Dkt. Mwinyi katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Naibu Abdi ambaye alisema kazi ya kwanza ni kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kubainisha kuwa, malipo yake kwa wanaCCM wenzake ni kufanya utumishi uliotuka kwa chama chao na kuhakikisha CCM inakuwa imara zaidi, inakuwa bora zaidi na inakuwa kimbilio la wanyonge na wananchi wa Zanzibar.
“Mimi na wenzangu tutafanyakazi kwa kutumia katiba zetu, kanuni zetu na miongozo mbalimbali iliyopo katika chama chetu ili kukifanya CCM kiendelee kushika dola na jukumu hilo litalifanya kwa weledi mkubwa na kwa umadhubuti, umakini, utii mkubwa na kuhakikisha CCM kila chaguzi inayohusu dola, tunajipanga vizuri, tunajisimamia vizuri na hatimaye tunashinda vizuri.
Hayo yanatokea wakati Pemba ambayo awali
ilitajwa kuwa ngome ya upinzani hususan CUF wakati huo hadi ACT Wazalendo hivi sasa kugawanyika kutokana na kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo inayofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.