Mbeto: ACT Wazalendo inakufa baada ya Oktoba 2025

0

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha ACT Wazalendo huenda kikafutika katika ulimwengu wa siasa baada ya Uchaguzi Mkuu 2025 kutokana na kukosa ajenda ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika kipindi cha Luninga cha Ana kwa Ana kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Zenjibari, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema katika mikutano yao yote wanamzungumzia Rais Mwinyi, kura ya mapema na simulizi za marehemu Maaalim Seif Hamad.

“Watu wanataka maendeleo sio propaganda na wanayaona mambo anayofanya Rais Dkt. Mwinyi, barabara hadi vichochoroni,” alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa, kutokana na maendeleo yaliyoletwa Zanzibar ndani ya kipindi alichokaa madarakani kila sekta imeguswa na wananchi hawana cha kumdai na ndio maana anasema ifikapo Oktoba mwaka huu 2025 ushindi ni asilimia 95.

Alisema, mathalani hivi sasa hakuna dawa inayokosekana katika hospitali zote tena bila malipo na suala la mgonjwa kuambiwa ‘kanunue dawa imebaki historia.’

Mbeto alishangaa chama hicho kuitisha mkutano na wanahabari na kuhoji iweje Rais akazindua jengo la kisasa la Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

“Hicho ndicho wanachotaka kusikia waZanzibari? Huko kuishiwa ajenda kwa kuwa kila kitu ameishafanya Dkt. Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia” alisema.

Dkt. Mwinyi ndio Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi atakapo kula kiapo Rais mwingine.

AMwenezi huyo alisema, kitendo cha kuzindua jengo hilo la kisasa lenye vifaa vyote muhimu na kumbi za kutosha ni sehemu ya majukumu yake na ACT kama wadau wa siasa walipaswa kushukuru sio kulaumu.

Mbeto alisema, ACT kushinda Urais Zanzibar ni ndoto, kwani muziki wa CCM ulimshinda hata nguri wa siasa Maaalim Seif Shariff Hamad ambaye aliwahi Katibu wa Uchumi na Mipango CCM naWaziri Kiongozi.

“Huyo mgombea wao wa Urais Zanzibar, Othman Masoud Othman mchanga sana kisiasa kwani hata kura atapiga kwa mara ya kwanza mwaka huu, hivyo hana jipya,” alisema Mbeto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here